Ufugaji Wa Kuku Wa Kienyeji - Part 3 - Mwisho

"....Ili ufanikiwe katika ufugaji wa kuku, ni muhimu sana kulifahamu vyemi kundi la kuku wako. Ukilifahamu vema kundi lako utaweza kuchagua kuku bora wa kuzalishia kwa kuangalia ubora wa wazazi wao."


KUSIMAMIA UFUGAJI WAKO

>>Kutunza kumbukumbu
Ili ufanikiwe katika ufugaji wa kuku, ni muhimu sana kulifahamu vyemi kundi la kuku wako. Ukilifahamu vema kundi lako utaweza kuchagua kuku bora wa kuzalishia kwa kuangalia ubora wa wazazi wao. Kufahamu historia ya afya ya kundi, kwa mfano:
• Umri ambapo vifaranga vilipata chanjo.
• Ni chanjo ya aina gani.
• Magonjwa ambayo yamewahi kushuambulia kundi, na dawa ulizotumia katika matibabu.
• ldadi ya kuku wanaokufa.
 Kukadiria kiasi cha chakula ambacho kuku wako watahitaji kwa muda fulani na aina ya chakula.
• Kujua kila siku kuku wametaga mayai mangapi.
• Kujua utahitaji muda gani kutunza kuku toka vifaranga mpaka wanapofikia kuuzwa.
Ili uweze kufahamu mambo haya yote unahitaji kutunza kumbukumbu.
Ufuatao hapa chini ni mfano rahisi wa kutunza kumbukumbu za kuku tangu wangali vifaranga mpaka wanapofikia uzito wa kuuzwa.

Mfano wa Kumbukumbu za ufugaji wa Kuku
i. Kumbukumbu ya Vyakula
Tarehe
Kiasi  cha
Chakula
Kundi  /  Umri  wa
Maoni (Gharama,

(Kilo)

kuku na idadi yao
Kimetumika kwa muda gani




nk)

15

Vifaranga












25

Wanaokua











Jumla










Hapa utaweza kujua wastani wa matumizi ya chakula kwa idadi ya kuku na kwa kipindi husika.

Tarehe ya kuuza……………………….
Idadi iliyouzwa……………………………
Umri wa kuku wakati wa kuwauza................
Mapato kutokana na kuuza……………………

ii. Kumbukumbu ya Kutibu Magonjwa
Tarehe
Magonjwa
Tiba
Maoni (vifo, gharama nk)




3.7.2009
coccidiosis
teramycin

5.9.2009
mdondo
furazolidone



















Kumbukumbu hii itakusaidia kujua magonjwa yanayosumbua mara kwa mara na kwa kipindi kipi. Pia na dawa inayosaidia zaidi kwa tatizo husika.

iii. Chanjo au Kudhibiti magonjwa
Tarehe
Ugonjwa/Wadudu
Dawa
Gharama




6.8.2009
Viroboto
Kunyunyiza doom powder au sevin powder

5.10.2009
coccidiosis
Amprol katika maji, kinga dhidi ya


















>>Jinsi ya Kufahamu Faida Unayopata
IIi uweze kufahamu faida unayopata kutokana na ufugaji wa kuku inakupasa kutunza kumbukumbu za matumizi na mapato ya kila siku.

Kwa mfano:
Upande wa matumizi ingiza
  Gharama ya kununua vifaranga (kama walitotolewa hapo hapo nyumbani inafaa ukadirie gharama hiyo).
  Gharama ya chakula.
   Kama unatengeneza na kuchanganya wewe mwenyewe kadiria kwa kutumia bei za viungo ghafi.
  Gharama ya mafuta ya taa (kama uliwakuza vifaranga kwa joto Ia taa).
  Gharama ya kusafisha banda kubadili matandazo.
  Gharama za madawa ya kinga (chanjo) na tiba.

Upande wa mapato ingiza mapato kutokana na:
Mauzo ya mayai.
Mauzo ya kuku hai.
Gharama ya mayai yaliyotumiwa nyumbani.
Mauzo ya mbolea kutoka katika banda.

Ufuatao ni mfano unaoonyesha jinsi ya kuingiza taarifa hizi katika daftari la kumbukumbu ya Kutibu Magonjwa
Tarehe
Matumizi
Sh.
Tarehe
Mapato
Sh.







Kununua vifaranga
6,000/=

Mauzo ya mayai 10
1,500/=

30 @ 200/=


@150/=


Kununua vyakula
1,500/=

Mayai na kuku
7,000/=

kilo 10 @150/=


waliotumiwa





nyumbani


Dawa ya kukohoa
1,500/=

Mauzo ya kuku 20
80,000/

1500/=


@ 4000/=


Dawa ya wadudu
1000/=

Mbolea iliyouzwa


1000/=





……nk.
….. nk

…. nk







Jumla













Baada ya kufanya mauzo yote ya kundi jumlisha matumizi yote na jumlisha na mapato yote katika kipindi kizima cha kufuga.

Ili kufahamu faida uliyopata fanya hesabu hii:
Jumla ya Mapato yote - Jumla ya Matumizi yote = Faida
>>Masoko
Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi yatakayomsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya:

Kwanza kabisa ajiulize kama bidhaa anayozalisha ina soko? Na kama soko lipo:
Lipo wapi na hali ya miundombinu za kulifikia iko vipi ( ili afahamu gharama ya kufika sokoni kama utaamua kuuzia sokoni).
Bidhaa inahitajika kwa wingi kiasi gani na wakati gani sokoni
Soko linahitaji bidhaa yenye sifa zipi ( ubora n.k. ili uzalishe sawa na matakwa ya soko n.k)
Kama wanunuzi watakuwa na utayari kununulia unakozalishia, je unao uwezo wa kutosheleza mahitaji yao (ili uweze kujipanga kukidhi mahitaji kwa kuongeza uzalishaji au kwa kuungana na wazalishaji wengine).
Linganisha bei ya bidhaa sokoni na bei ya kuuzia unakozalishia (ili ujue palipo na faida zaidi kwako baada ya kuondoa gharama za kufuata soko) Ila ukiamua kuuzia sokoni hakikisha unao uwezo wa kushindana na wauzaji wengine huko sokoni.

Majibu ya maswali haya ndiyo yatakayokupa msingi wa kujipanga kiuzalishaji ili hatimaye upate faida. Hivyo hata kabla hujaanza kuzalisha fahamu haya yaliyotajwa hapa juu. Kutafuta na kutumia taarifa za masoko ya sehemu tofauti
Kwa kadri utakavyokuwa unaendelea kuzalisha, mabadiliko mbali mbali yatatokea kuhusiana na uzalishaji wako na hata kuhusiana na soko la bidhaa unayozalisha kwa maana ya kuku. Ili uendane na mabadiliko yanayotokea ni muhimu mzalishaji upate taarifa za hali ya soko mara kwa mara. Taarifa hizi zitakusaidia kufanya maamuzi yatakayokuwezesha kuendelea kupata faida.

Taarifa za masoko zinaweza kupatikna kwa wazalishaji kadhaa kuungana na kuunda umoja wao. Katika umoja huo wawakilishi wachache wanakuwa na jukumu la kutafuta taarifa za masoko ya kuku sehemu mbali mbali ambako kunaweza kuwapa wazalishaji tija zaidi. Walio katika umoja huo watatumia taarifa hizo kufanya maamuzi ya kuuza kwa faida zaidi kwa pamoja au kwa mmojammoja kutegemeana na hali halisi. Watoa taarifa pia watafanya mawasiliano ya kuwajulisha wanunuzi juu ya upatikanaji wa kuku kwenye maeneo wanakozalishiwa.
>>Mbinu zaidi ya kupata masoko mazuri
*Umoja wa kuzalisha na kuuza
Kwa kawaida kama bidhaa ina soko, wateja hupatikana kwa urahisi pale wanapohakikishiwa upatikanaji wa bidhaa kwa wingi katika sehemu moja. Katika hali hii, wanunuzi huwa tayari hata kununua kwa bei ya juu zaidi kwa sababu ya kupunguza muda na gharama ya kutafuta bidhaa ya kutosha kupeleka sokoni.a

Kwa upande wa kuku jambo hili linawezekana kama mfugaji atafuga kuku wengi wa umri usiopishana sana kwa wakati mmoja. Watakapofikia kimo kinachofaa kuuza utawauza wengi kwa wakati mmoja na kwa faida zaidi. Mahali ambapo mfugaji mmoja mmoja hawezi kukidhi wingi wa hitaji la wanunuzi, wafugaji kadhaa wanaweza kuunda umoja wao wa kuzalisha (kila mmoja kwake ) na kuuza kwa kipindi kimoja na kupata faida zilizotajwa hapa juu.

Faida nyingine ya kuuza katika umoja ni kuongezeka kwa uwezo wenu wa kupanga na kusimamia bei mnayotaka kuuzia. Sauti na uamuzi wenu wa pamoja utawapa nguvu ya kusimamia bei yenu mnayoipanga dhidi ya bei za chini wanazotaka wanunuzi. Uwezo wako wa kusimamia bei unyoitaka ni mdogo ukiuza peke yako.
  
 Wasiliana nasi ikiwa utakutana na chamngamoto yoyote. Nakutakia mafanikio katika Ufugaji wako wa kuku!

Comments

Top Jobs that others viewed

JOB VACANCIES: AGRICULTURE

JOBS: VET and Animal Health Officers