Ufugaji Wa Kuku Wa Kienyeji - Part 3 - Mwisho
"....Ili ufanikiwe katika ufugaji wa kuku, ni muhimu sana kulifahamu vyemi kundi la kuku wako. Ukilifahamu vema kundi lako utaweza kuchagua kuku bora wa kuzalishia kwa kuangalia ubora wa wazazi wao." KUSIMAMIA UFUGAJI WAKO >>Kutunza kumbukumbu Ili ufanikiwe katika ufugaji wa kuku, ni muhimu sana kulifahamu vyemi kundi la kuku wako. Ukilifahamu vema kundi lako utaweza kuchagua kuku bora wa kuzalishia kwa kuangalia ubora wa wazazi wao. Kufahamu historia ya afya ya kundi, kwa mfano: • Umri ambapo vifaranga vilipata chanjo. • Ni chanjo ya aina gani. • Magonjwa ambayo yamewahi kushuambulia kundi, na dawa ulizotumia katika matibabu. • ldadi ya kuku wanaokufa. • Kukadiria kiasi cha chakula ambacho kuku wako watahitaji kwa muda fulani na aina ya chakula. • Kujua kila siku kuku wametaga mayai mangapi. • Kujua utahitaji muda gani kutunza kuku toka vifaranga mpaka wanapofikia kuuzwa. Ili uweze kufahamu mambo haya yote unahitaji kutunza k...